Kama ilivyo benki nyingi zinatoa huduma za kibenki kwa kupia namba maalum za USSD ( mfano *150*09# n.k), Sasa tunaanza kuona benki kadhaa zikiwapa wateja wake nafasi ya kupata huduma zao kupitia application “Apps” kwa wale wenye smartphone kama Samsung as iPhone

Wakati nikiwa na shauku kubwa ya maendeleo haya makubwa, nikiwa na nia ya kuanza kuwasilisha mikakati ya kidijitali kuongeza mauzo katika sekta hii ya uchumi na fedha, nakutana na changamoto kadhaa katika sekta hii:

 • Ni benki mbili tu Tanzania zipo kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, mtandao wenye watanzania zaidi ya laki 5, mtandao unatoa suluhisho la bei nafuu sana kwenye kutoa huduma za papo kwa papo kwa wateja
 • Benki nyingi bado zinapendelea mfumo wa kujitangaza kwenye magazeti, radio na “Billboards” tu wakati kuna watanzania millioni 11.3 (zaidi ya Asilimia 25 ya Tanzania nzima) wanatumia intaneti kila siku.
 • Tovuti za benki nyingi Tanzania hazifunguki wala kutumika vizuri kwenye simu, wakati aslimia 75% ya watumiaji wote wa intaneti Tanzania hutumia simu zao kuliko Kompyuta.
 • Bado huwezi kufunga au kujisajili benki kwa njia ya mtandao. Mahitaji, kanuni na taratibu ni nyingi sana na zinaleta vikwazo. Kwa mfano, ulazima wakutoa vielelezo vya makazi, wakati unaweza kujiunga na mfumo wa “Mobile money” (m-pesa, tigo pesa, airtel money) kwa urahisi Zaidi.
 • Mauzo ya kidijitali hutoa suluhisho la bei nafuu la kuvutia wateja wapya kujiunga na benki yako vilevile husaidia kupunguza gharama za kuwasiliana na wateja ambao tayari wapo kwenye benki yako.

  Vielelezo vya picha vilivyotumika hapo chini vimepatikana kupitia vyanzo vya taarifa tunavyotumia hapa Squad Digital kila siku kwa ajili ya wateja wetu na kuwashauri kuhusiana na mikakati ya mauzo kidijitali.

  Tazama ni jinsi gani benki zetu hapa Tanzania zinavyolingana katika masuala ya kidijitali kama vile; kurasa za jamii, “search engine optimization” (Nafasi iliyopo benki pale mteja anapoingia mtandaoni kutafuta taarifa za mabenki Tanzania), “Website user experience” (Maoni ya watumiaji wa Tovuti za mabenki) na “Digital PR” (Uwepo wa mabenki mtandaoni kwa ujumla)

  Je umeridhika na uwepo na matumizi ya Mtandao ya Benki yako? Tuambie ni huduma zipi unafurahia, hupendelea au ungependa kuziona zikihamia mtandaoni kutoka kwa benki yako.

  Banks-Tz-Infograph-Revised